Tukio hilo la kusikitisha limetokea saa 12 jioni huko mwera Wilaya ya Magharib A Unguja mwanamama huyo aliyepewa kichapo ambae jina lake limehifadhiwa pamoja na muhalifu alie mfanyia unyama huo.
Wakati mama huyo alipofuatwa ili kueleza mkasa huo sababu gani iliyo mfanya ata akapata majeraha hayo lakini hakuweza kuzungumza kutokana na majeraha aliyoyapata.
Hata hivyo waandishi wa habari wamefanikiwa kupata maelezo kutoka kwa mtoto wa mama huyo ambae amesema kuwa babaake alimpiga mamaake kwa kosa la kumfikiria kuwa amekwenda kwa mwanamme na sio mara ya kwanza kumfanya kitendo kama hicho.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda msaidizi mwandamizi wa jeshi la Polisi Hassan Nassir Ali ametoa wito kwa wanandoa kuwa si tabia nzuri kufanya tabia kama hiyo. na kwawale ambao wanajitoa mishipa yafahamu kwa kutenda makosa kama hayo hatua kali zakisheria zitawafikia juu yao.
Hadi sasa mtuhumiwa huyo ameshatiwa mikononi mwa Polisi.