Aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuiana Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali nyingi zisizolingana na kipato chake, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka 44
Baadhi ya mashtaka aliyosomewa Gugai anayedaiwa kumiliki viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano pamoja na pikipiki, ni pamoja na kutakatisha fedha, kughushi fedha pamoja na kudanganya kuhusu mali anazomiliki.
Gugai alijisalimisha mwenyewe hapo jana baada ya TAKUKURU kutangaza dau la milioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake, kwani walikuwa wakimtafuta bila mafanikio.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi