Meya aweka wazi alichoambiwa polisi


Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia CHADEMA Jacob Boniface ambaye jana alishikiliwa na polisi, ameweka wazi sababu ambayo jana ilimsababishia kukamatwa na jeshi la Polisi na kulala ndani, huku uchaguzi ukiendelea

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Meya Jacob amesema yeye alikuwa ni msimamizi wa vituo vya kupigia kura ambayo ipo kisheria, lakini baada ya muda alishangaa kuona polisi wanakuja kumkamata kwa tuhuma ambazo hazikuwa za kwlei.
“Nilikuwa nasimamia uchaguzi kama msimamizi wa uchaguzi wa chama changu, nikiwa kituoni nashangaa kuona nakuja kukamatwa na polisi, nilipofika kule wakaniambia kuwa wamepata taarifa kwamba nimejipanga kufanya vurugu na wenzangu, kitu ambacho sio kweli”, amesema Jacob Boniface.
Meya huyo ambaye ni miongoni mwa viongozi machachari wa CHADEMA amesema mpaka sasa hajajua hatma yake kama anapelekwa mahakamani au la, kwani aliachiwa huru majira ya saa saba usiku baada ya kulipa dhamana, huku uchaguzi ukiwa umeshakwisha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo