Na. Ahmad Mmow.
WAKATI mgogoro ukiendelea kurindima ndani ya CUF-Chama Cha wananchi. mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Seleman Bungara (Bwege) nikama ameweka chumvi kwenye kidonda kwa kumtuhumu mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, profesa Lipumba kuwa amesababisha chama hicho kumegeka vipande viwili.
Bwege aliyasema hayo juzi alipofanya mahojiano maalumu na blogi hii(Muungwana) kutoka Dodoma, baada ya kuombwa aeleze hatima na maajaaliwa ya kugombea tena ubunge mwaka 2020.
Alisema licha ya kuwa nimapema kuzungumzia uchaguzi ujao iwapo atagombea tena mwaka 2020. Lakini chama hicho kinapita katika wakati mgumu nakusababisha hata wenye tamaa ya kuomba ridhaa kwa wananchi ili wachaguliwe tena hawajui hatima yao.Kwasababu ya mgogoro huo ambao alidai umesababishwa na profesa Lipumba.
Bwege ambae katika mazungumzo hayo alimfananisha na kumuita mwenyekiti mwenyekiti huyo ni adui mwenye sumu kali inayoweza kuuwa nguvu na ushirikiano wa vyama vya upinzani vyenye nia ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini, alisema mwenyekiti huyo anaetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya smash amesababisha chama hicho kugawanyika na kupatikana vyama viwili ndani ya kimoja.
"Wote tuna kumbuka kwamba profesa Lipumba aliacha mwenyewe nafasi ya uenyekiti, aliombwa sana asifanye hivyo. Lakini hakusikia akatimkia Rwanda Kwamadai ya kusutwa na nafasi yake kutokana na Lowassa ambae alimshawishi mwenyewe aje katika upinzani kuwa mgombea wa Urais na viongozi wenzake ndani ya chama kumuona kikwazo. hivyo atabaki kuwa mwanachama tu , "alisema Bwege.
Mbunge huyo aliendelea kumsakama profesa Lipumba kwa kusema mwenyekiti huyo dhamira yake ya kugombea Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)kugonga mwamba, na baada ya kufanikiwa juhudi zake za kuhakikisha Dkt Wilbroad Slaa asifanywe kuwa mgombea, yeye (profesa Lipumba) na mmoja wa viongozi wa NCCR-Mageuzi ndio waliokwenda kumshawishi Lowassa ajiunge kwenye chama chochote kilichokuwa kwenye UKAWA.
"alitambua kwamba mpango wake wakuwa mgombea uligonga mwamba akaenda kushinikiza kwenye chama chetu awe mgombea tukamkatalia. Tuliheshimu makubaliano, nakwakweli tunaweza kujipongeza kwa kitendo cha kumkatalia. Kwasababu kwa vitendo anavyofanya nidhahiri angetuvuruga katika kipindi cha uchaguzi, "Bwege alizidi kumwaga mchele kwenye kuku wengi.
Mbunge huyo ambae alikiri hayupo kwenye kambi inayomuunga mkono mwenyekiti huyo ambae mara kadhaa amekuwa akiweka wazi kwamba anaendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa mujibu na matakwa ya Katiba ya chama hicho,alisema sababu zinazoelezwa na mwenyekiti huyo hazina ukweli. Bali ameamua kudhoofisha nguvu za upinzani kwa masilahi yake. Kwakusaidiwa na watu wasiopenda mabadiliko.
Alisema nijambo la kushangaza kusikia mwenyekiti alisema nafsi ilimsuta kutokana na kuwepo mgombea aliyemtafuta mwenyewe. Huku akisema ilikuwa nijambo lisilo wezekana pande zote mbili za muungano wagombea watoke CUF.Ukweli ambao profesa Lipumba alikuwa anaujua.
"Wengi hawajui mambo haya wanasema Lowassa aliletwa na mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe na alipewa fedha. Sio kweli kabisa, Lowassa aliletwa na Lipumba katika UKAWA kimkakati,"Bwege alizidi kuanika mambo.
Profesa Lipumba pamoja na kujibu na kueleza mara kwa mara sababu za kuondoka na kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti, lakini Muungwana ilitaka kujua maoni na mujibu ya tuhuma na lawama za mbunge huyo. Hata hivyo Haku jibe, hata baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa simu hadi habari hii inaandikwa.