Kiongozi mwingine aliyeswekwa ndani na DC

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva ameeleza kuwa mpaka sasa mtendaji wa mtaa huo anashikiliwa na jeshi la Polisi, na Kwamba wamepokea taarifa kuwa Mwenyekiti wa mtaa huo Denis Moyo amekimbia na hivyo amempa siku mbili ajisalimishe mwenyewe kwenye kituo cha Polisi Cha Temeke

Kwamujibu wa mkazi wa eneo hilo Mohamed Mmeya amemueleza DC Lyaniva kuwa walipojaribu kufuatilia kwa watu waliokuwa wakikata miti hiyo walijibiwa kuwa viongozi hao wa Serikali ndio waliotoa vibali vya kuvuna miti hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke SSCP Muhudhwar Msuya amethibitisha kuwashikilia watu 10 akiwemo mwanamke mmoja katika tukio hilo, na kwamba wamewakuta na mashine moja ya kuchania magogo na kwamba wanaendelea na upelelezi na mahojiano.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo