Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Vicent Mashinji ametupa jiwe gizani na kudai kwamba kitendo cha dola kumkamata mtu kwa tuhuma za uchochezi ni udhaifu wa serikali katika kujibu hoja
Dr. Mashinji amesema kwamba siasa zenye msamiati wa uchochezi huwa hazipo hivyo kwani wadhaifu huwa ndiyo wanaotumia mabavu na siyo hoja.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dkt Mashinji ameandika "Najenga hoja, unasema mi mchochezi. Kweli umekosa ushawishi jitafakari upya, siasa za sasa msamiati wa uchochezi haupo. Ni hoja kwa hoja!"
Hivi karibuni viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakikamatwa na jeshi la polisi mara kwa mara kwa tuhuma za uchochezi.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi