Rekodi hiyo imewekwa na mpanda milima mashuhuri duniani kwa kutumia baiskeli Juanito Oiarzabal, ambaye amekuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro kwa baiskeli akitumia saa 31 ndani ya siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Katika rekodi hiyo mpya Juanito aliambatana na wenzake wawili Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia ambao walianza kupanda pamoja mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika kupitia lango la Kilema.
Kwa upande wake meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete amesema hatua hiyo ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru ni ishara nzuri kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa 