Msichana mwenye umri wa miaka 16 aliediriki kumtupa mtoto wake jaani usiku wa manane bila ya kujali afya ya kichanga hicho usiku huo huko Donge mtambile wilwya ya Kaskazini B Unguja.
Akamatwa na kuhemea katika Hospitali ya kivunge kwa matibabu baada ya kujifungua huku akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati kichanga hicho kimeshapelekwa nyumba ya kulelewa watoto mazizini.
Akithibitishwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kaimu Kamanda Mkoa wa Kaskazini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 16 amaekamatwa wakati amekimbilia hospitali ya kivunge kwa matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya baada ya kujifungua.
Kaimu Kamana huyo amesema kuwa msichana huyo amejifungua kwa kujificha na baadae kumtelekeza mototo jaani kwani ni kitendo ambacho ni cha kusikitisha sana.
Amesema mpaka sasa mtuhumiwa huyo yupo chini ya ulinzi wakati amelazwa hospitali ya kivunge kwa matibabu na baada yahapo hatua za kisheria zitachukuliwa juu yake.