Zitto Kabwe aachiwa huru

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam

Mwanasheria wa Zitto Kabwe amesema kuwa mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015 hivyo mwanasheria anasema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama watakwenda mahakamani. 
Kwa upande wake Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa mahakamani ili waweze kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo. 
"Tunasubiri ni lini watatupeleka mahakamani kwa ajili ya kutetea masuala ambayo tumezungumza lakini ya ziada ni kama ambavyo Mwanasheria amezungumza kwa hapa ni makosa mawili ya Sheria ya Takwimu na Sheria ya makosa ya mitandao, wananchama waendelee kuwa watulivu tu kwa sababu kila mtu alitarajia kuwa tutakamatwa kwa kuwa Rais alisema kuwa nikamatwe hivyo tusingekamatwa ningeshangaa, la ziada ni kwamba tusubiri mahakamani itakuaje" alisisitiza Zitto Kabwe 
Mbali na hilo kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka wanachama pamoja na viongozi wa chama hicho kuendelea na harakati za uchaguzi mdogo wa udiwani na kusema endapo wakishinda katika uchaguzi huo ni kitu ambacho kitakuwa faraja kwao. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo