Akiongea na waandishi wa habari Katibu wa CCM Wilaya Kinondoni Bw. Hannaf Msabaha amesema kuwa tayari wamepata taarifa kuwa wapo wagombea wameanza kutoa pesa elfu kumi kumi kuwahonga wapiga kura ili kupata nafasi hizo na kusema kuwa tayari wametoa taarifa katika vyombo husika kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo.
"Tumeshapata taarifa kuwa kuna baadhi ya wagombea wameanza kufanya matendo ambayo yanakiuka taratibu, kanuni na katiba yetu wameanza kupita na kutoa toa pesa shilingi elfu kumi kumi kwa wapiga kura kwa njia za simu, jambo hilo tumeshalikabidhi kwa mamlaka zinazohusika ikiwepo TAKUKURU atakapokamatwa au kubainika sisi hatutasita kutoa taarifa kwa mamlaka zilizowateua kutengua uteuzi wao au kuwafutia huo uteuzi hata kama uchaguzi umeshaisha, au hatakama mtu alishachaguliwa tutawaengua na tutaanza upya" alisisitiza Hannaf
Aidha Katibu huyo wa CCM aliwataka wagombea hao kuacha kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
