Rais Magufuli: Nipo tayari Kubadilisha sheria ili kuwalinda wananchi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema yuko tayari kubadilisha sheria ili kuweza kuwalinda wanachi wanaotakiwa kupitiwa na bomoa bomoa mkoani Mwanza, kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege na miundo mbinu mingine

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia taifa kwenye sherehe za uzinduzi wa daraja la Furahisha la mkoani Mwanza, na kusema kwamba serikali yake haiko tayari kuona watu wakionewa , hivyo yuko tayari kuwalinda hata kwa kubadilisha sheria itakayowaruhusu wananchi hao waendelee kuishi hapo.
"Tuliwatazama watu wakajenga wakaweka 'Investment' zao, sasa leo tunawafukuza, tusubiri kwanza, inawezekana walifanya makosa lakini kwa sababu serikali yangu ina huruma nasema ndugu zangu msiwabomoleshe, yapo maeneo ambayo kwa kweli itabidi watu wahame, mfano wale wa uwanja wa ndege, kama kuna mahali pa kubadilisha sheria mimi nitazibadilisha ili kusudi baadhi ya wananchi waliojenga pale miaka 30 tuweze kuwalinda na kukaa pale na kuendesha maisha yao", amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli leo yupo mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo pia licha ya uzinduzi wa daraja la Furahisha, anatarajiwa pia kuzindua kiwanda kimoja.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo