Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Mgufuli amemhamisha kituo cha kazi Dkt Binilith Mahenge kutoka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Kuwa mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Rais Magufuli ametangaza mabadiliko hayo leo wakati akiwaapisha makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu wa wizara, na wakuu wa mikoa sita leo Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Awali Rais Magufuli amemteua Christina Mdeme kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Jordan Rugimbana kabla ya kubadilisha na kumtana Mdeme kuripoti Ruvuma ambapo atakuwa mkuu wa mkoa huo kuchukua nafasi ya Dkt Binilith Mahenge ambaye amemhamishia Dodoma