Mwenyekiti wa Halmashauri atishia Kuua

Herode Jivava.

MAKAMU Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduma, Herode Jivava ametiwa nguvuni na Polisi akidaiwa kutishia kuua kwa maneno.

Jivava ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Songwe anakuwa kiongozi wa nane kukamatwa na kuwekwa mahabusu. Baadhi ya waliokamatwa  wamefunguliwa kesi mahakamani na wengine wako nje kwa dhamana wakisubiri upelelezi wa polisi kukamilika.

Akizungumza kuhusu kukamatwa kwa Jivava, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo amesema alikamatwa jana Jumapili jioni mjini Vwawa akijiandaa kuingia uwanjani kuangalia mpira na alipelekwa Kituo cha Polisi Tunduma.

“Asubuhi hii tumefika hapa Polisi tumeambiwa Jivava anatuhumiwa kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno. Eti aliwatishia mgambo wakati wakiwaondoa kwa nguvu Machinga mjini Tunduma,” amesema.

 Sikagonamo amesema wanamsubiri mwanasheria ili kushughulikia suala hilo. Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange hakuwa tayari kuzungumzia taarifa za kukamatwa kwa Jivava.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo