Mrithi wa Kigwangalla aanza kazi Rasmi

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile, amesema ataendeleza mipango ya serikali ya kuboresha sekta ya afya kwa kuhakikisha changamoto mbalimbali zinatatuliwa ikiwemo ya tatizo la dawa na na suala zima la matatibu.
Dkt. Ndugulile amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akihojiwa na kipindi cha East Africa Breakfast, kinachorushwa na East Africa Radio wakati akielezea vipaumbele vyake mara baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo hapo Oktoba. 7, na kuapishwa hapo jana
Naibu Waziri huyo amesema kuwa vipaumbele vingine ambayo atashirikiana na watumishi wingine wa wizara hiyo ni kuhakikisha anapunguza vifo vya kina mama na watoto pamoja kushughulia changamoto ya watumishi hasa maeneo ya pembembezoni.
Aidha ameongeza pia atashughulikia suala zima la kukamilisha mchakato wa Bima ya afya kwa wote kutokana na gharama za matibabu kwa sasa kuwa juu zaidi hivyo kwa kutumia bima itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama hizo.
Dkt. Faustine Ndugulile amechukua nafasi ya Dkt. Hamisi Kigwangala baada ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri jumamosi iliyopita.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo