Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema kuwa watu wasiojulikana watajulikana baada ya kukamatwa na kuwa suala la mbunge wa jimbo la Singinga Mashariki Tundu Lisu linafanyiwa uchunguzi na jeshi la polisi kama yalivyo matukio mengine.
Kuwa mtu anayepanga kufanya uhalifu huwa hafiki polisi kujitambulisha kuwa ana kwenda kufanya uhalifu ndio maana akifanya uhalifu anaitwa mtu asiyejulikana ila akikamatwa hujulikana .
“ Watu wasio julikana ni matumizi tu ya lugha ila wakikamatwa hujulikana na hawaitwi wasiojulikana tena ,tunaendelea kuwasaka hao wanaojiita watu wasiojulikana hata kule Kibiti waliokuwa wakifanya mauwaji walikuwa ni watu wasiojulikana baada ya kuwakamata ni watu wanaojulikana “
IGP Sirro aliyasema hayo leo mjini Iringa wakati akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili kwa ziara yake ya kikazi mkoani hapa, kuwa suala la Lisu kila siku amekuwa akiulizwa na wanahabari kuhusu upelelezi wake umefikia wapi ila kwao jeshi la polisi wanaliona tukio hilo ni sawa na matukio mengine .
“ mimi sio mwanasiasa hili ni tukio kama yalivyo matukio mengine na Lisu ni mtanzania kama wengine hivyo jeshi la polisi linaendelea kulifanyia uchunguzi suala hilo kama yaliyo matukio mengine ,kila siku maswali ni juu ya Lisu ila niwaambie kuwa hili ni tukio la kama matukio mengine tunaendelea na uchunguzi “
Alisema kuwa suala hilo la Lisu limekuwa likizungumzwa kila wakati ifahamike kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na kitengo cha upelelezi na hategemei kufundishwa kazi na mtu juu ya nini afanye katika suala hilo .
Hata hivyo alisema kuwa kwa upande wake ana weledi ndani ya jeshi la polisi na haoni changamoto yeyote kufanya kazi na wanasiasa kwani wanasiasa mi sehemu ya jamii na wanafanya siasa kwa mujibu wa sheria ila wakikiuka sheria wanawajibika kwa mujibu wa sheria .
“ Kwa hiyo hakuna mwanasiasa aliye juu ya sheria akiuka sheria atawajibika kwamujibu wa sheria na atashughulikiwa kama mtu mwingine yeyote hivyo hakuna mwanasiasa atakayenisumbua mwanasiasa atakayetoa lugha ya matusi atakamatwa tu kazi yangu ni rahisi sana kwa kuwa nasimamia sheria .
Aidha IGP Sirro aliwataka askari wa usalama barabarani kutumia busara zaidi katika kazi hiyo badala ya kuwapiga faini madereva pasipo kuwapa onyo kuwa kufanya hivyo si sahihi .
Alisema pamoja ipo dhana potofu miongoni mwa jamii kuwa askari hao wa usalama barabarani huwa wanapangiwa kiasi cha pesa kwa ajili ya kukabidhi kwa siku jambo ambalo si kweli kwani hakuna anayempangia pesa za kukusanya askari zaidi ya kumataka kusimamia sheria za usalama barabarani .
“ Hakuna askari wa usalama barabarani anayepangiwa makusanyo ya faini IGP ni mmoja nchi hii mimi ndio IGP nasema hakuna IGP anayepangia askari wa usalama barabarani pesa labda wana IGP wao nyumbani kwao “
Kuwa kazi ya askari hao wa usalama barabarani ni kusimamia sheria za usalama barabarani na sio kila kosa ni la kumpiga mtu faini lazima busara itumike ikiwa ni pamoja na kumpa onyo mhusuka pamoja na elimu kabla ya kukimbilia kumpiga faini .
“ Jambo la kwanza la kuzuia uhalifu ni elimu kwanza siku ya pili onyo na siku ya tatu ni faini sio unaanza kwa faini pasipo kumpa elimu wala onyo , ila wakati mwingine hawa polisi si malaika yawezekana wametoka nyumbani wakiwa ovyo hivyo wanahamishia hasira zao kwenye faini ila naomba muwaelewe hawa ni watoto wetu tuwasamehe bure ila ninachosisitiza elimu kwanza ukiona dereva kaongeza spidi kwanza mpe elimu kwanza ”
Kuhusu uboreshaji wa nyumba za askari polisi nchini alisema kuwa kuna programu maalum ya kuboresha makazi ya askari polisi kupitia fedha wanazopata .
“ Nimefurahi sana kuwafahamu nimekuwa nikisoma tu nondo zenu ila leo nimewafahamu ahsanteni sana ila naombeni jaribuni kuandika kile ambacho nimesema kuna mmoja jana Mbeya ameandika IGP anasema wana Siasa wasiongee hii si kweli mimi siwezi kuwazuia wanasiasa kuongea wazungumze tu ila wasivunje sheria”
Kuhusu kauli mbali mbali ambazo amekuwa akiziandika kwenye mitandao ya kijamii Mange Kimambe alisema kuwa kauli zake hizo zimekuwa zikivunja sheria ndani ya nchi ila nini ambacho jeshi la polisi lina mpango gani hawezi kusema kwa sasa .
|