Afanya mauaji kisa deni la Umeme

Kijana Mmoja aliyejulikana kwa jina la Wilson Mwasi mwenye umri wa miaka kati ya 28 na 30 ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtoto wa mwenye nyumba anayoishi kwasababu ya kudaiana pesa ya kulipia umeme.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa tano usiku huko Mwananyamala mtaa wa Kopa wilaya ya Kinondoni ,inadaiwa kabla ya mauaji kijana aliye sababisha kifo alifika nyumbani kwao na kuanza kutoa maneno kwa wapangaji kuwa hawalipi umeme.
Mashuda wa tukio hilo wamesema baba wa marehemu aliamua kumtuliza kijana huyo asiendelee kutoa matusi lakini kijana huyo alianza kumsukuma na ndipo Marehemu Wilson akaingilia kati baada ya kuona baba yake anasukumwa hali iliyopelekea kijana mwenye nyumba kuchukua kisu ndani na kumchoma Wilson.
Marehemu alifariki wakati akiwa njiani anakimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.
Mama mzazi wa kijana aliyesababisha mauaji amesema kwa masikitiko kuwa anaiachia serikali ichukue hatua juu ya tukio lililotokea ingawa kijana wake alianza kulalamika kuhusu kulala giza bila umeme lakini anadai alimnyamazisha na kumtaka aingie ndani lakini hakutaka kuingia.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo