Humphrey Polepole amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter alipoweka ripoti ya 'World Economic Forum' ambayo inaonyesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa barani Afrika, tofauti na hao watu wachache ambao wamekuwa wakipinga na kusema uchumi wa Tanzania haukuwi.
Kufuatia bandiko hilo la Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole baadhi ya watu wameendelea kupinga kwa kusema hali ya maisha mtaani ni ngumu huku wengine wakidai huo uchumi unaosemekana kukuwa Tanzania hauna uhalisia na maisha ya kawaida ambayo watu wanaishi.
