Siwezi kuiomba radhi CCM - RPC Geita


RPC wa Geita,  Mponjoli Mwabulambo amefunguka na kusema yeye hawezi kuomba radhi kwa CCM mkoa wa Geita na kusema endapo itathibitika kweli amekidhalilisha chama hicho kama ambavyo wanadai baadhi ya viongozi mkoani humo yupo tayari kuacha kazi yake

Mponjoli amesema kuwa yeye anaamini kila jambo alilofanya lilikuwa sahihi kwa kuwa viongozi hao walikuwa wanafanya uhalifu na kusema yeye anaona viongozi hao ndiyo walikuwa wakitaka kukudhalilisha Chama Cha Mapinduzi ila si yeye. 
"Siwezi kuomba radhi tena hilo nimethibitishie kabisaa niombe radhi kwa lipi mbona nimewaambia, mimi nidhalilishe Chama Cha Mapinduzi kwa lipi? Wao walisimama kama watetezi wa chama au watu wa kubomoa chama?" alihoji Mponjoli 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo