Mashine yetu itarudi barabarani ikiwa timamu kabisa – Mhe. Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mhe. Lissu hajawahi kata kauli tangu siku ya kwanza alipopata shambulio la kupigwa risasi huku akisema kuwa watu wasiwe na hofu mashine yao itarudi barabarani ikiwa timamu kabisa.
Mbowe amezungumza hayo leo Ijumaa alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matibabu ya Lissu yanayoendelea jijini Nairobi wakati akiwaeleza waandishi wa habari.
“Wale tuliomuona hatua za kwanza nataka kusema Mhe. Lissu hakukata kauli mpaka anaingia theatre kuna watu waliexagulate kuwa Mhe. Lissu alikata kauli pamoja na majeraha yote Mhe. Lissu hajawahi kukata kauli ambacho nataka wananchi waeleweni tofauti kati ya kukata kauli na kupewa dawa za usingizi unapata maumivu mpaka unalazwa kwa nguvu kutokana na wingi wa majeraha aliyokuwa nayo hiyo ndo hali iliyomtokea,” alisema Mbowe.
“Mhe. Lissu lakini fahamu zake ziko timamu kabisa, akili zake ziko timamu kabisa, ufahamu wake uko 100% nataka niwahakikishie kabisa mashine yetu itarudi barabarani ikiwa sahihi na timamu kabisa.”
Mbowe alishambuliwa kwa kupigwa risasi Septemba 7 Mjini Dodoma na watu wasiojulikana eneo la ‘area D’ .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo