Kupona kwa Lissu iliandikwa - Nyalandu

Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amesema kitendo cha Tundu Lissu kusalimika kifo kwenye tukio la kupigwa risasi ni Mungu tu ndiye aliandika, lakini kinamuumiza zaidi huku akilaumu ameikosea nini nchi mpaka kufanyiwa hivyo



Lazaro Nyalandu ameyasema hayo kwenye ukurasa wake wa facebook, akiwa mkoani Mbeya ambapo alishiriki maombezi ya Tundu Lissu ambayo yalifanyika siku ya jana. 
"Nimekuja Mbeya kulikumbusha Taifa kuwa kupigwa kwa mmoja wetu ni kupigwa kwetu sote, kuumizwa kwake ni kuumizwa kwetu sote, na kudhulumiwa kwake huyo mmoja ni dhuluma dhidi ya kila Mtanzania. Tundu Lissu amepona kwa kuwa imeandikwa, naamini, ndani ya moyo wake akiwa katika maumivu lukuki aliyonayo, atakuwa anajiuliza nimekukosea nini Tanzania", ameandika Lazaro Nyalandu
Lazaro Nyalandu amekuwa miongoni mwa watu wanaofuatilia kwa karibu matibabu ya Tundu Lissu jijini Nairobi, huku akiimiza watanzania kuendelea kumuombea ili aweze kupona kabisa na kurejea kwenye hali yake ya kawaida.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo