Polisi Tarime yatumia risasi za moto kumdhibiti..............


Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya lililazimika kutumia risasi za moto kumdhibiti mtu mmoja ambaye alivamia Bank ya NBC usiku akidaiwa kuingia baada ya kutoboa ukuta.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya Henry Mwaibambe amesema Jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu mtu huyo ambaye hakufahamika jina wala umri ambaye alivamia Bank hiyo mara mbili.
>>>”Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio la ajabu kidogo. Tarehe 19, Saa Sita na dakika Nne usiku, mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake wala umri amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na Askari Polisi waliokuwa kwenye lindo la Bank ya NBC.” – Kamanda Mwaibambe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo