Nyumba ya Mama Anne Mkapa kuvunjwa

Nyumba inayoaminika kumilikiwa na mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Tanzania Benjamini Mkapa itavunjwa ili kuruhusu upanuzi wa barabara ya Morogoro.
Nyumba hiyo ya Anne Mkapa itakuwa miongoni mwa maelfu ya nyumba ambazo zinatarajiwa kuvunjwa , shughuli itakayowaathiri zaidi ya watu 10,000.
Gazeti la Th Citizen lilitembelea nyumba hiyo inayodaiwa kumilikiwa na Bi Anne na mwanamke mmoja aliyepatikana katika eneo hilo alithibitisha kwamba ni nyumba ya Mkapa.
“Natoka familia ya Mkapa, lakini siwezi kusema mengi kuhusu suala hili, iwapo mnataka maelezo zaidi ni muhimu kuwasiliana naye,” alisema mwanamke huyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo