Ndoa ya Nuh Mziwanda na mkewe Nawal ilioyofungwa mwaka jana Novemba imeingiwa na kidudu mtu kilicholeta madhara na kupelekea ndoa hiyo kuvunjika.

Akiongea katika U-Heard ya Clouds FM, Jumatano hii Nawal amethibitisha kuachana na baba mtoto wake Anyagile na kila mtu anaishi maisha yake na wakati huyo huo amesema tayari yeye ameshaolewa na mwanaume mwingine.
” Sina mume mimi, Nuh wakati anaamua kurudi kwenye dini yake (Ukristo) hakunishirikisha kwa chochote na mimi sasa hivi nipo kwa bibi yangu Msasani, pia nimesha olewa na mtu mwingine,”amesema mrembo
Pia Nawal amedai kuwa mpaka sasa ameondoka alipokuwa anaishi na mumewe wake huyo, huku akidai mumewe ndio alikuwa na makosa katika ndoa hiyo pia tangia aondoke hapo amekuwa hamjali mtoto wao kwa chochote kile pia Nawali ameeleza kuwa anauwezo wa kumlea mtotot wake bila ya msaada wake kama aliweza kumzaa mwenyewe.