Mashabiki wa Simba wameanza kuingiwa na wasiwasi na timu yao

Zikiwa zimebaki siku 5 watani na wa jadi Simba na Yanga wakutane katika mchezo wa ngao ya jamii tarehe 23 Agosti 2017 kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018 mashabiki wa Simba wameanza kupagawa.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wameanza kuwa na wasiwasi na uwezo wa  Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog baada ya jana timu hiyo kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu la Mlandege katika Uwanja wa Amaan Zanzibar timu ambayo juzi ilifungwa bao 2 dhidi ya Yanga.

Kufuatia matokeo hayo na uwezo walioonyesha Simba wapo baadhi ya mashabiki wamemnyooshea kidole kocha huyo kuwa hafai na kudai hana uwezo, kwa kuwa Simba sasa inawachezaji wengi wazuri na wenye uwezo wa hali ya juu hivyo wanasema timu haikustaili kupata matokeo hayo.

Klabu ya Simba imecheza mechi kadhaa za kirafiki ambazo ni maandalizi kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara na matokeo yake kwa kila mechi ilikuwa kama ifuatavyo.

Simba SC 0 - 0 Mlandege
Simba 1 - 0 Mtibwa Sugar
Simba 1 - 0 Rayon FC ya Rwanda
Simba Sc 1 Vs 1 Bidvest Fc ya Afrika Kusini
Simba 0-1 Orlando Pirates ya Afrika Kusini




JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo