MAAJABU YA MTI KATEMBO, UPANDE UTOMVU MWEUPE, UPANDE DAMU! Mti huu ni aina ya Mvule na unapatikana katika Kijiji Cha Lugombo, Kata ya Kisiba, Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya. Mti huu, maarufu kwa jina la Mti wa Katembo, unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 600 au zaidi. Ukubwa wake wa duara unahitaji watu kuanzia wanane waliounganisha mikono. ukiupima una futi 39 katika kimo cha juu kidogo lakini una futi 43 chini kabisa.
Inaelezwa kuwa Mnamo mwaka 1975 mti huu kwa mara ya kwanza ulidondosha tawi lake moja ambalo, hata ukifika leo panaonekana, inasemekana lilipoanguka ilikuwa kama tetemeko la ardhi kutokana na kishindo kilichotetemesha kijiji kile na vijiji jirani.
