Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba mkoani Songwe imeagiza kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh.Frank Mwakajoka kwa tuhuma za kuwadhihaki wateule wa Rais.
Kamati ya Ulinzi na usalama wilayani ya Momba imeagiza kiongozi huyo kukamatwa baada ya kumdhihaki Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Juma Said Irando.
Mbunge huyo baada ya taarifa kusikika kuwa anatakiwa kukamatwa kwa amri ya Kamati ya Ulinzi alituma ujumbe mfupi kupitia mitandao yake ya kijamii akilalamika juu ya suala hilo.
"Kwanini Wabunge nikiwa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi kwenye kesi ya Mh Haonga nimekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Momba, akidai nilimsema na kumdhalilisha ndani ya kikao cha baraza la Madiwani mji wa Tunduma kilicho fanyika hivi karibuni" alisema Haonga
Afisa habari wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Tunduma
"Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Mhe. Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi Viwawa, kwa amri ya Mkuu wa wilaya kwa mujibu wa OCD" alisema Tumaini Makene.