Breaking News: Tundu Lissu Aifungukia IMMMA Advocates Kuchomwa Moto


Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Tundu Lissu amewataja watu wanaodaiwa kulipua ofisi za Immma Advocates zilizopo Barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

Lissu amesema kwamba watu waliovalia sare za polisi, wakiwa na silaha na madumu ya petroli, walivamia ofisi hizo usiku, wakawateka walinzi kabla ya kulipua bomu na kutokomea kusikojulikana.

Aliendelea kueleza kwamba lengo la watu hao lilikuwa ni kuharibu nyaraka muhimu zinazotumiwa na mawakili wanaoongozwa na Fatma Karume na Laurence Masha kwenye kesi mbalimbali zinazoendelea mahakamani, ikiwemo kesi ya Kampuni ya Acacia.

Ofisi hizo zilivamiwa usiku wa saa nane, Agosti 26 ambapo walinzi wawili waliokuwa lindo kwenye ofisi hizo, walitekwa, wakanyweshwa kitu kinachodaiwa kuwa ni sumu na kwenda kutupwa Kawe huku ofisi hizo zikilipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu. Angalia video hii hapa chini LIVE:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo