Wafanyabiashara wa kata ya Tandala wilayani Makete mkoani
Njombe wametakiwa kutambua soko huria la kufanya biashara hivyo kuacha kasumba
ya kuwaandama wafanyabiashara wanaofanya biashara zao kwa kuamua kupunguza bei
Akizungumza na wafanyabiashara hao hii leo, Diwani wa
kata ya Tandala Mh Egnatio Mtawa amesema mara nyingi serikali inawaacha
wafanyabiashara wafanye bishara zao kwa uhuru lakini pale wanapolazimika kuuza
bidhaa kwa kiwango kilichopitiliza serikali haitasita kuingilia kati
Amesema katika siku za hivi karibuni amepokea malalamiko
ya baadhi ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa kwa bei ya chini kuandamwa na
wafanyabiashara wengine kwa madai kuwa wanawaharibia soko, jambo ambalo
amelikemea na kutaka kila mfanyabiashara auze bidhaa zake kwa bei anayoona
inafaa lakini isipitilize kiwango cha juu kilichopendekezwa na serikali
Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wetu baada
ya kusikia yaliyojiri kwenye mkutano huo baina ya diwani na wafanyabiashara
wametoa maoni yao
Katika hatua nyingine Diwani Mtawa amewataka wananchi
kuchangamkia fursa pindi itakapojengwa kambi kwa ajili ya wakandarasi
wanaotengeneza barabara ya lami kutoka Makete kwenda Njombe huku akiwaonya
wafanyabiashara kununua bidhaa za wizi ama za magendo ikiwemo mafuta na saruji
kuacha suala hilo kwa kuwa ni kinyume cha sheria na endepo wakibainika
watachukuliwa hatua
Pia amewataka wafanyabiashara kuacha kufanya udanganyifu
kwenye biashara zao kwa kigezo cha kulipa mapato madogo kwa mamlaka ya mapato
nchini TRA
Sikiliza zaidi sauti hizi hapa chini:-
