Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka
ameagiza watumishi wote wanaotuhumiwa kufanya ubadhilifu wa Milioni 120 katika
halmashauri ya Makete ambao bado wapo kazini wasimamishwe mara moja
Pia Mkuu huyo wa mkoa ameagiza watumishi wanaotuhumiwa ambao wamehamishwa warudishwe Makete na wengine walioacha kazi wasakwe
na warudishwe kujibu tuhuma zinazowakabili
Akizungumza kwenye baraza maalum la madiwani leo lililokuwa likijadili hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali zilizoonesha
kuwa halmashauri ya wilaya ya Makete imepata hati ya Mashaka, Mkuu huyo amesema
hakuna mtumishi hata mmoja aliyejihusisha na ubadhilifu wa fedha hizo za maendeleo
atakayepona
Mbali na hilo Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza
kuwepo kwa mahusiano mazuri baina ya watendaji wa halmashauri na waheshimiwa
madiwani kwa kuwa ushirikiano wao utaepusha changamoto mbalimbali zinazoikabili
halmashauri ya wilaya ya Makete kwa sasa
Bonyeza hapo chini usikilize ripoti hii kama ilivyoripotiwa na kituo cha Redio Green FM 91.5:-