Atiwa Mbaroni Kwa Kujifanya ni Mkurugenzi wa Habari IKULU

Mfanyabiasha Ramadhani Athumani Juma maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kujitambulisha   kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu, Gerson Msigwa.

Amesema hati ya mashtaka jana wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori alidai kuwa kati ya Juni 28 na Julai 4,2017 Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya alijitambulisha kama Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu kwa Ladslaus Matindi.

Amedai  kuwa mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Mshtakiwa alikana shtaka upande wa mashtaka ulidai upelezi bado haujakamilika, Mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya sh 1 milioni.Kesi imeahirishwa 23,8,2017 na mtuhumiwa  hajakamilisha masharti hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo