Dida hatasaini mkataba YANGA na juhudi za kumbembeleza zimekwama


Kauli iliyotolewa na Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali kuwa wameachana na kipa wao Deogratius Munish ‘Dida’ imeonyesha kuwashitua mashabiki wengi wa klabu hiyo.

Wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Dida kuondoka na wengine wakimtaka kuvuta subira.

Lakini wako mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiutaka uongozi wa Yanga kukaa na kumalizana naye vizuri.

Wengine wameshauri kama amepata timu nje aende lakini si hapa Tanzania.

Pondamali alisema Dida aliwaambia hatasaini mkataba na juhudi za kumbembeleza zimekwama.

Hivyo kipa wa African Lyon waliyemsajili, Beno Kakolanya waliyenaye na watasajili kipa mwingine chipukizi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo