Watanzania zaidi ya asilimia 86 hawana vyeti vya kuzaliwa.

Zaidi ya asilimia 86 ya watanzania hawana vyeti vya kuzaliwa hali inayotajwa kuathiri utoaji huduma kwenye mifumo serikali ikiwemo upangaji wa maendeleo, elimu, uchumi, makazi na afya.

Takwimu hizo zinatolewa na waziri wa katiba na sheria profesa paramagamba kabudi katika mjadala wa maboresho ya usanifu mpango wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu na ukusanyaji wa takwimu (crvs) ambapo anasema kwa kujibu wa sensa ya watu na makazi 2012 idadi hiyo ya watu haina vyeti ya kuzaliwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakala wa usajili udhamini na ufilisi profesa hamis dihenga anasema hali hiyo inachangiwa na mtazamo hasi ulioanza tangu enzi za ukoloni pamoja nausajili wa sasa kuwakatisha watu tamaa kutokana na sababu mbalimbali.

Itv inazungumza na wakazi wa mkoa wa dodoma na kupata maoni yao kuhusu umuhimu wa cheti cha kuzaliwa ambao wanadai bado hakuna hamasa kutoka serikalini na watu huamasika kutafuta nyaraka hizo endapo wanahitajika kufanya hivyo tu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo