Edward Lowassa Afunguka Alivyohojiwa na DCI, Aachiwa kwa Dhamana

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amefunguka kuhusu alivyohojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi  wa Makosa ya Jinai (DCI) ambapo baada ya kuhojiwa ameachiwa kwa dhamana na kuondoka makao makuu ya polisi majira ya saa 8.

Akizungumza nyumbani kwake, Oyster Bay jijini Dar mara baada ya kutoka Makao Makuu ya Polisi, Lowassa amesema aliitwa kuhusu kauli aliyoitoa ya viongozi wa dini ya Kiislam wa Zanzibar (Uamsho) kuendelea kusota rumande kwa miaka kadhaa sasa kauli ambayo inadaiwa kuwa kuwa ni ya uchochezi.

“Nimeitwa kuhojiwa kuhusu hotuba niliyoitoa hivi karibuni wakati wa futari kwa Mbunge Waitara. wengine wameielewa kama ni ya uchochezi.

“Nimejieleza wachakuchua maelezo yangu ambayo wanayatafakari hivyo tutakutana tena Alhamisi saa 6:00 mchana.
“Hivyo niwatake wanachama wa Chadema wasiwe na hofu, tupo imara.” alisema Lowassa

Wakati wa futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) Lowassa alisema aliwaahidi wananchi endapo angechaguliwa kuwa rais angewatoa mashehe hao siku hiyo hiyo lakini anashangaa viongozi hao wa dini wanavyoendelea kusota rumande mpaka sasa bila kufahamu kosa lao.

Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.

Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge huyo.

“Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu  wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika maelezo ya onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” amesema Kibatala.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo