Siku chache baada ya bweni la wasichana shule ya
sekondari Mbalatse wilayani Makete mkoani Njombe kuunguzwa na moto, uongozi wa
shule hiyo bado unaendelea na jitihada zake za kuhakikisha bweni hilo linarejea
katika hali yake ya kawaida
Hatua hiyo itasaidia wanafunzi kuendelea kutumia bweni
lao badala ya kulala madarasani kama ilivyo sasa ikizingatiwa kuwa bado wiki
chache shule iweze kufunguliwa baada ya likizo kumalizika
Akizungumza kupitia kituo cha redio Green Fm Shuleni hapo hii leo makamu Mkuu
wa shule hiyo Mwl. Yohana Pilla amesema
licha ya changamoto ya moto uliounguza vifaa vya wanafunzi hao Juni 16 mwaka
huu, wameendelea kuwatia moyo wanafunzi hao na kubainisha kuwa mpaka sasa
wanaendelea vizuri baada ya tukio hilo
Aidha mwalimu huyo amewaomba wananchi kwa kadri
watakavyojaliwa kuisaidia shule hiyo kwa hali na mali kwa kuwa hivi sasa
wanatakiwa kupata vitu vipya vya wanafunzi baada ya baadhi kuunguzwa na moto
yakiwemo magodoro
Usiku wa Juni 16 Mwaka huu bweni la wasichana katika
shule hiyo ya sekondari liliwaka moto ambao mpaka sasa chanzo chake
hakijajulikana moto ambao ulizimwa mapema kabla haujaleta madhara makubwa zaidi
Bonyeza play ya sauti hizo hapo chini umsikilize:-
Bonyeza play ya sauti hizo hapo chini umsikilize:-