skip to main |
skip to sidebar
Hizi ndizo sababu ya ajali iliyouwa wanafunzi 32
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga alisema eneo la ajali lina kona nyingi na mteremko mkali na kwamba, kuna maeneo ambayo yamekuwa yakisababisha ajali kutokana na miundombinu yake ilivyokaa.
Aliyataja eneo jingine kuwa lipo barabara ya Morogoro kwenda Dodoma linaloitwa Makunganya lina utelezi mwingi na kuwasihi madereva kuwa makini sana wakati wa mvua. Wanafunzi waliofariki ni wa darasa la saba.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro alisema miili ya wanafunzi hao itaagwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi