Kamati ya Bunge pia imemsamehe Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kosa la kudharau Mamlaka ya Bunge April 4, 2017. Mbunge mwingine ni Ester Bullaya ambaye amepewa karipio baada ya kukiri kosa lake sawa na Mbowe.
BAADA YA MJADALA
Kupitia vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea Makao Makuu Dodoma, leo Jumanne Wabunge wa pande zote bila kujali itikadi za vyama vyao, wamemwomba Spika kutoa msamaha kwa Mbunge Halima Mdee aliyepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobakia.
Baada ya Wabunge kwa umoja wao kuomba kiti cha Spika kutompa adhabu hiyo Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Bunge limetangaza kumsamehe na ataendelea na vikao kwa sharti la kutorudia tena kosa.