Wizara ya kilimo mifugo na Uvuvi imetakiwa kutoa kauli
bungeni ni lini itaendeleza shamba la mifugo la Kitulo lililopo wilayani Makete
mkoani Njombe ili liwe na manufaa ya kutosha kwa wananchi wa makete na taifa
kwa ujumla
Akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha
2017/2018 Hii jana jumamosi Bungeni Dodoma mbunge wa jimbo la Makete Prof Norman Sigalla
amesema endapo waziri wa kilimo mifugo na uvuvi hatatoa majibu ya kumridhisha
basi atashika shilingi
Amesema shamba la Kitulo linauwezo wa kuchukua ng'ombe
4,500 lakini mpaka sasa lina ng'ombe 750 tu licha ya waziri aliyekuwepo wakati
huo Mwigulu Nchemba kufika katika shamba hilo na kuahidi kutolewa bilioni 7.6
lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wa hilo
Aidha Mbunge huyo ameiomba serikali kuangalia kwa jicho
la pekee wakulima wa wilaya ya Makete hasa wa Viazi na Pareto ambao amesema
hawanufaiki kwa kiwangi kikubwa na kilimo hicho kwa kuwa bado hali ya soko
haiko vizuri kwao
Amesema nchi jirani ya Kenya inakuwa vizuri kwa kilimo
cha viazi kwa kuwa wamejipanga vizuri ili hali wapo wakulima wa viazi katika
wilaya ya Makete ambao pia wanahitaji kutoka kwa kusaidiwa na serikali
Unaweza kumsikiliza vizuri kwa kubonyeza play hapo chini:-
