Updates: Polisi watinga eneo walipovamiwa wana CUF Leo

Polisi inawahoji wanachama wa CUF waliovamiwa na watu waliovaa ‘mask’ katika ukumbi wa Vina Hoteli, Mabibo leo.

Polisi imeshafika eneo la tukio na inawahoji wanachama hao wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad waliokuwa wakifanya mkutano wao wa ndani.

Pia Polisi inawahoji waandishi wa habari waliopo eneo la tukio.

Inaelezwa kuwa watu wanne, waliovaa soksi nyeusi usoni (mask) walivamia mkutano huo wa CUF wakiwa na mapanga na bastola.

Tutaendelea kukujuza yanayoendelea kuhusu habari hii.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo