Mh.Majidi ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani kuwa makini na utendaji wao wa kazi huku akipokea mifuko ya Cement 400 kutoka kwa wadau wa maendeleo na kuagiza mifuko hiyo kupelekwa kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa,vituo vya afya na ujenzi unaondelea wa kituo cha polisi Lugoba na kuwataka viongozi kuwa wasimamizi wa mifukohiyo.
Mapema mkurugenzi wa halmashauli ya Chalinze Bw. Edes Lukoa amesema watendaji wote kwa sasa wanahitaji kujipima katika utendaji wa kazi kabla ya kuchukuliwa hatua huku afsa elimu Sekondari Bw.Timothy Bernard akitoa taarifa za wanafunzi walioripoti shuleni kuwa ni 2435 kati ya wanafunzi 2522 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na 87 mpaka sasa hawajaripoti na wengine kuanza kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwepo wazazi wao kupelekwa Mahakamani.
