Mzee huyo anayeishi kata ya Ibaga Kijiji cha Ilongo kitongoji cha Ilangida amemjeruhi binti huyo mwenye umri wa miaka 14
Tukio hilo lilitekelezwa Tarehe 21 Aprili mwaka huu ambapo mzee huyo alianza kumpiga binti huyo kwa fimbo na baadaye kuchukua Kuni yenye moto na kuanza kumuunguza,sehemu za matiti,usoni na inasemekana kaunguzwa sehemu za mapaja
Mama wa mtoto alipotaka kumtetea binti yake naye alipigwa,na kuchomwa kwa kuni hiyo yenye moto shavuni.
Binti huyo alifichwa ndani na baba ,baada ya siku tatu hali ya binti haikuwa nzuri wanafamilia wakaanza kutoa taarifa kwa majirani.
Hatimaye chanzo chetu kinaeleza kuwa taarifa hizo zikafika kituoni cha polisi Ibaga ,ambapo askari wa jeshi hilo walifika nyumbani kwa mzee huyo na kushuhudia binti huyo akiwa ndani na hali yake hiyo ya majeraha.
Binti akapelekwa kituo cha afya Makalama kwa ajili ya matibabu, mpaka sasa mgonjwa yupo Hospitalini hapo huku akiwa hawezi kuzungumza,