Mkuu wa
wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy amewaomba wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza
kwa wingi kuupokea mwenge wa uhuru unaotarajiwa kuwasili wilayani hapa Mei Mosi
mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu huyo wa wilaya
amesema maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru kwa mwaka huu 2017 yanaendelea
vizuri ambapo mwenge huo unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo,
sanjari na kuungana na wafanyakazi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
duniani ambavyo vyote vitafanyika siku moja
Mh Kessy amesema mwenge huo utapokelewa eneo la Kimani
katika kata ya Mfumbi ukitokea wilaya ya Wanging'ombe na kuwaomba wananchi
kujitokeza katika maeneo yote utakakopita sambaba na eneo la Mkesha ambapo ni
stendi ya Iwawa Makete mjini
Aidha mkuu huyo wa wilaya amezungumzia umuhimu wa kutunza
mazingira hasa vyanzo vya maji, ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa
Makete pamoja na maeneo jirani yanayotegemea maji kutoka wilayani Hapa
Hata hivyo amewapongeza wananchi wa Makete kwa kubomoa
kwa hiari nyumba zao zilizokuwa zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara, kupisha
ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami toka Njombe hadi Makete, na kuwaomba
wananchi kuendelea kuwa na subira licha ya kusikia ahadi za ujenzi wa barabara
hiyo kwa muda mrefu bila kutekelezwa, lakini sasa muda wa utekelezaji umewadia
>>>Bonyeza Play hapo chini uweze kumsikiliza
