Wazazi walioandamana kupinga mwalimu mkuu kuvuliwa madaraka

Jeshi la polisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamekutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wazazi zaidi ya 100 waliokuwa wanaandamana kuelekea katika shule ya sekondari ya Tabaruka kwa madai ya kutoridhishwa na uamuzi wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kumshusha madaraka mkuu wa shule hiyo na kuwa mwalimu wa kawaida.

Bila kujali mvua iliyokuwa ikinyesha,wazazi hao wameandamana kupinga agizo la Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema Boniphace Magesa la kumvua madaraka mkuu wa shule ya sekondari tabaruka mwalimu dotto ndemela, kwa madai kwamba kufanya hivyo ni kuzidi kuzorotesha maendeleo ya kitaaluma yaliyokuwa yamefikiwa katika shule hiyo.

Malalamiko ya wazazi wa shule hiyo juu ya kuvuliwa madaraka kwa Mkuu wa shule hiyo Dotto Ndemela,pamoja na Jeshi la polisi wilayani humo kutumia mabomu kuwasambaratisha wananchi hao yanatolewa ufafanuzi na mkuu wa wilaya ya sengerema emmanuel kipole.

Aliyekuwa mkuu wa shule hiyo Dotto Ndemela anadaiwa kukiuka maelekezo yaliyozuia uhamisho wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kutolewa kabla ya mwezi Machi mwaka huu, ambapo mkuu wa wilaya hiyo Emmanuel Kipole amesema tume aliyoiunda kumchunguza mkuu huyo wa shule,imegundua kuwa ameingiza wanafunzi zaidi ya 35 kinyume cha utaratibu bila kupata kibali cha mkuu wa mkoa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo