Wakazi wa Njombe wahimizwa kuchangia damu

Katibu Tawala wilaya ya Njombe, Joseph Chota amewahimiza wakazi wa mkoa wa Njombe kujitolea kuchangia damu salama ili kusaidia watu wenye mahitaji.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa katika maadhimisho ya wiki ya matendo ya huruma ya kanisa la Waadventista Wasabato mkoni Njombe, Chota amesema damu itakayochangwa pia itasaidia kukabiliana na tatizo la uhaba wa damu salama katika bohari za dawa hospitalini.

Waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato Duniani kote huadhimisha siku ya matendo ya huruma kwa kuisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ni sehemu ya ibada na kumtukuza Mungu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo