Polisi auawa Kinyama Baada ya Kuitiwa Mwizi

Watu sita wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumuua askari polisi Abdala Chande kwa kumkata na mapanga baada ya kupita katika nyumba inayofanyika biashara  ya pombe haramu ya gongo eneo la Msaranga manispaa ya Moshi.

Kamanada wa polisi mkoa wa  Kilimanjaro ACSP Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kusema kuwa ivigenge vingi vya pombe haramu ya gongo vinahifadhi wahalifu.

Amesema askari huyo alishambuliwa na mapanga baada ya watuhumiwa hao kumwona akipita karibu na nyumba hiyo akiwa kwenye shughuli zake ndipo walipo piga kelele za kumuita mwizi na kuanza kumshambulia na mapanga.

Katika tukio lingine Jeshi hilo linawashikilia  watu 13 kwa tuhuma za  mauji ya ya kumnyonga mwanamke Anita kimario na kisha kuufukia mwili wake katika mashamba ya miwa ya kiwanda cha sukari cha TPC Moshi.

Hata hivyo kamanda Mutafungwa amewataka wananchi mkoani Kilimanjaro kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkono na kwamba kwa sasa wameelekeza nguvu kwenye nyumba zinazojihusisha na utengenezaji wa pombe haramu ya gongo ambazo zinasadikiwa kuhifadhi wahalifu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo