Polisi afariki Dunia baada ya kuanguka kwenye Gari



Konstebo Dotto (28) amefariki dunia papo hapo baada ya kuanguka kwenye gari la polisi eneo la  Nyang’oro, Tarafa ya Isimani mkoani hapa alipokuwa kazini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi  amesema tukio hilo lilitokea juzi jioni wakati askari huyo na wenzake walipokwenda kufanya doria eneo hilo.

“Ni kweli tumepatwa na msiba, askari wetu akiwa kazini na wenzake jana jioni alipata ajali, alianguka kwenye gari na kufariki dunia. Tunajiandaa na utaratibu wa kuusafirisha mwili wa marehemu kwa maziko nyumbani kwao mkoani Tabora,” amesema Mjengi.

Alisema mwili wa askari huyo aliteleza kutoka kwenye gari na kuanguka barabarani.

Wakati huohuo, vijana wa bodaboda katika Kijiji cha Ushirika, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamelaumiwa kwa kuanzisha vurugu zilizosababisha wakazi wa eneo hilo kuyakimbia makazi yao baada ya polisi wawili kujeruhiwa na gari lao kuvunjwa.

 Diwani wa Mpuguso, Jerad Bakize alisema vurugu hizo zilisababisha wananchi kuyakimbia makazi yao baada ya polisi kuanza kurusha mabomu na kuwasaka wahusika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo