Nay wa Mitego amuibukia Waziri Mwakyembe Wizarani

Siku kadhaa zimepita tangu msanii Nay wa Mitego kuachiwa huru, ambapo alikuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za wimbo wake wa ‘WAPO’ kudaiwa kutokuwa na maadili.
Msanii Nay wa Mitego aliachiwa huru baada ya agizo lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ambapo aliomba aonane na Nay wa Mitego ili kumshauri vitu vya kuongeza kwenye wimbo wake wa ‘WAPO’. Sasa jioni hii Nay wa Mitego amefika Dodoma wizarani kwa ajili ya kuonana na Dk. Mwakyembe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo