Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, March 27, 2017 kutoa agizo kwa Jeshi la Polisi kumuchia huru msanii wa Bongo Fleva Nay wa Mitego na kutaka wimbo wake ‘Wapo’ uchezwe kwenye vyombo mbalimbali.
Sasa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter hakuweza kuficha hisia zake juu ya maamuzi ambapo aliyaandika haya……>>>>> “Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!” – Ney wa Mitego.