Mtu mmoja alie julikanwa kwa jina la Akbar ambaye alikuwa ametoweka nyumbani kwa masaa kadhaa amekutikana akiwa amekufa ndani ya tumbo la chatu.
kwa mujibu wa polisi Akbar alitoweka siku ya Jumapili katika kisiwa cha Sulawesi, baada ya kuondoka nyumba akienda kuvuna mawese katika shamba la familia yao.
Mashura ambaye ni msemaji wa polisi katika mkoa wa Sulawesi Magharibi aliiambia BBC, kuwa wanavijiji waliripoti kwa polisi kuwa Akbar hajaonekana kwa muda wa saa 24 Kisha polisi walianza kumtafuta nakugundua kuwa amemezwa na chatu huyo.
Chatu huyo ambae ana urefu wa mita saba alipopasuliwa tumbo, mwili wa mwanamume huyo ulipatikana ndani.
