Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Mwanasheria wa wilaya ya Makete Godfrey Gogadi akitoa elimu kwa washiriki
Akizungumza Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya
Makete Bw.Godfrey Gogadi katika ukumbi wa Shirika la SUMASESU uliopo kata ya
Tandala amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa maelekezo na kufundisha utendaji
kazi wa mabaraza ya kata ambapo wamekutanishwa watendaji wa vijiji,watendaji wa
kata, wenyeviti wa vijiji na viongozi wa mabaraza ya kata pamoja na wasaidizi
wa kisheria.
BW.Godfrey amewataka viongozi hao kuyaishi yale
waliyofundishwa katika mafunzo hayo na pale inapotokea inahitajika ushauri
katika maamuzi ni vema wakatafuta washauri kwani nia ya serikali ni kuona
mabaraza ya kata ya wilaya makete yanatenda haki.
Pia amewataka wananchi kuyatumia mabaraza ya kata kwa
kutoa malalamiko yao ili waweze kutafutiwa suluhisho la malalamiko yao.
Mafunzo hayo yamewakutanisha viongozi kutoka tarafa ya
lupalilo ikijumuisha kata ya Tandala ,ukwama mang'oto na Lupalilo
Msikilize Mwansheria huyo akizungumza:-




