Wazee wawili wambaka mtoto wa miaka 14

Wazee wawili wajitoa mshipa wa fahamu wambaka kwa zamu mtoto mwenye umri wa miaka 14 jina limehifadhiwa na kumsababishia mumivu makali.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Tasani Makunduchi wilaya ya kusini Unguja wazee hao waliofahamika kwa jina la Ramadhan Issa Simai (55) na mwenziwe  Ali Suleimani Ameir (43) wote wakaazi wa Tasani Makunduchi ambapo walimbaka kwa zamu mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali.
Nae mzazi wa mtoto huyo amesema mmoja wa wazee hao alifika nyumbani na kumpa pesa mtoto huyo kumbe ndio mtego wa kumfanyia unyama huo na kusema kuwa hana ujamaa na waliomharibia mwanawe hivyo hatua kali za kisheria zichukuliwe zidi yao
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi kamishna msaidi wa polisi Juma Saadi Khamis amelaani kitendo hicho na kusema kuwa  wazee hao tayari wameshatiwa mikononi mwa polisi kwa kuchukuliwa hatua za kisheria


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo